kampuni inafanya kazi za uwakala kwenye mali zisizo hamishika kwa kushirikiana na mamlaka za kiserikali katika miji ambayo kampuni inafanya shughuli zake.

Pia Pamoja na kushirikiana na taasisi za serikali kampuni yetu inatoa huduma hizo kwa watu binafsi na taasisi zisizo za kiserikali,kwaajili ya kuhakikisha kunakuwepo na muunganiko sahihi kati ya wahitaji na soko.

Kwa mfano kampuni imekwisha wahi kufanya huduma hii ya uwakala na jiji la Dodoma kwa utaratibu wa kuvitangaza viwanja vya jiji kupitia kampuni kwa dhumuni la kuviuza kwa wateja kwa utaratibu maalumu wa kugawana asilimia% na serikali kama sehemu ya malipo ya kazi hiyo,

Hata hivyo utaratibu huu siyo kwa jiji tu hata kwa watu binafsi au taasisi binasi, utaratibu katika kipengele hiki upo kimazungumzo Zaidi na makubaliano, hakuna kiwango cha moja kwa moja kutokana na mazingira ya biashara na aina ya biashara