Cheo | Majukumu |
---|---|
WAKURUGENZI | kampuni ya Jumaco Property limited ina jumla ya wakurugenzi 2 ambao kwa Pamoja ndio wanashiriki katika kufanya maamuzi ya juu ya kampuni,hiyo haimanishi kuwa kampuni inaendeshwa kwa mtazamo wa watu wachache la hasha bali kampuni ya Jumaco Property Limited ni miongoni mwa makapuni yanayojali na kuheshimu michango na maoni ya kila mtumishi wake bila kujali nafasi yake kwenye kampuni. Kampuni inawachukulia watumishi wake wote kama familia moja yenye malengo na maono ya Pamoja maamuzi katika kampuni hufanywa kwa njia ya ushirikishwaji hii inasaidia watumishi kujua vizuri majukumu yao na kuwa na ufahamu juu ya kwanini wanatakiwa kufanya kazi kwa bidi kubwa. |
MENEJA WA KAMPUNI | Nafasi ya meneja wa kampuni hii ni moja kati ya nafasi nyeti katika kampuni, ni nafasi inayowakilisha wakurugezi wa kampuni katika maeneo ambayo kampuni inatoa huduma zake, meneja wa kampuni analo jukumu la kuhakikisha malengo ya kampuni yaliyopangwa yanafikiwa kwa wakati ili meneja wa kampuni aweze kusimamia majukumu yake vizuri anapaswa kushirikiana na uongozi Pamoja na timu yake anayoiongoza kuona kwa Pamoja namna nzuri ya kufikia malengo ya kampuni Pia meneja wa kampuni anao wajibu wa kuhakikisha mapato ya kampuni yanaakuwa sambamba na huduma bora kwa wateja meneja anao wajibu wa kuwajengea uwezo watumishi anaowaongoza kwa kuratibu mafunzo mbalimbali yatakayowajengea uwezo watumishi wake. |
AFISA MWAJIRI | Hii ni nafasi muhimu katika kampuni ili kampuni ifanikiwe inahitaji watu ni kazi ya afisa mwajiri kuchagua watu sahihi kulingana na taaluma na uwezo wao, afisa mwajiri anaowajibu wa kuchunguza uwezo na kipaji cha kila mwajiliwa ili apange kazi kulingana na taaluma na uwezo binafsi wa mwajiliwa. Afisa mwajili anawajibu wa kuwaendeleza waajiriwa wake kiuwezo ili kusaidia kukuza uwezo wa watumishi wake hivyo kuongeza uzalishaji wenye tija kwa maslahi mapana ya kampuni. |
WAPIMAJI | Hii ni timu ya wataalamu inayohusika moja kwa moja katika swala zima la upimaji wa maeneo ya kampuni Pamoja na maeneo ya wateja wenye uhitaji wa kupimiwa; timu hii hufanya kazi kwakushirikiana na halimashauri ya jiji na manispaa na wilaya kwa kufuata mipango au matumizi ya aridhi iliyopangwa pia hii ni timu inayoishauri taasisi juu ya mipango na malengo endelevu ya maeneo ya kampuni. |
MAAFISA MAUZO | Maafisa mauzo ni timu ya wataalamu inayofanya kazi kubwa ya kutangaza na kuuza huduma na bidhaa zetu kwa wateja ni timu yenye ufahamu na uelewa wa miradi yetu mbalimbali ni timu iliyopitia mafunzo mbalimbali juu ya huduma kwa wateja, pia wanao uwezo wa kutoa ushauri juu ya mali zisizo hamishika. |